Juhudi za kutaka kumbandua gavana Kawira Mwangaza zachacha

  • | Citizen TV
    3,925 views

    Bunge la kaunti ya Meru limefanya kikao cha kukusanya maoni ya umma kuhusu mswada wa kumbadua gavana Kawira Mwangaza. Kizaazaa kilitanda bungeni huku wanaomuunga mkono gavana Mwangaza na wanaotaka abanduliwe wakivuruga mkutano. Baadhi ya walalamishi walituma nyaraka kuwasilisha mapendekezo yao. Haya yakijiri, mahakama ya Meru itasikiza na kutoa maagizo kwenye kesi iliyowasilishwa na gavana Mwangaza kupinga kujadiliwa kwa hoja ya kumbandua. Gavana huyo anatarajiwa kufika bungeni kesho kujitetea.