- 4,327 viewsDuration: 1:00Seneta wa Nairobi Edwin Sifuna amesema ni sharti kamati inayosimamia utekelezaji wa agenda kumi zilizokuwa msingi wa ushirikiano wa chama cha ODM na uda itoe taarifa kamili hapo kesho ambapo itakuwa ni mwaka mmoja tangu kutiwa saini kwa mkataba huo. Sifuna amesema shughuli hiyo haipaswi kuahirishwa wala mkataba kubuniwa upya, akitaka kila kitu kiwekwe hadharani, siyo katika mikutano ya faragha kati ya ODM na UDA.