Wakazi wa eneo la Urudi wapanda miti kaunti ya Kisumu

  • | Citizen TV
    673 views

    Wakazi wa eneo la Urudi lililoko Nyakach kaunti ya Kisumu walishiriki zoezi la kupanda miti ili kuzuia mafuriko mto Nyando ambayo husababisha uharibifu na hasara katika mashamba yao. Akizungumza kwenye hafla hiyo, mkuu wa eneo la Nyakach Peter Mutu ametoa wito kwa wakazi hao kupanda miti kwa wingi ili kuimarisha mazigira kufuatia agizo la rais. Afisa wa msitu kaunti ya Kisumu Isaack Sabule alisema wanalenga kupanda miti billioni tano kwa muda wa miaka mitano ili kuzuia maporomoko ya udongo eneo hilo kutokana na mafuriko