Rais amemsuta Raila kwa kuandaa maandamano ya kupinga serikali

  • | K24 Video
    95 views

    Rais William Ruto sasa amesema kinara wa upinzani Raila Odinga ana uhuru wa kufanya maandamano kama anavyotaka. Rais amesema haya katika kaunti ya Embu alikohudhiria ibada ya pamoja. Raila Odinga ametishia kuandaa maandamano kutokana na hatua ya muungano wa kenya kwanza kufurusha makamishena wanne wa IEBC, huku Justus Nyangaya akiamua kujiuzulu. Aidha, rais na naibu wake Rigathi Gachagau wamesema hawatahadaiwa na kinara wa Azimio kufanya handisheki, Gachagua akisema makubaliano kati ya Uhuru na Raila ndiyo yaliosababisha kuvurugika kwa ajenda za maendeleo ya serikali ya awali. Raila amepanga kufanya mikutano ya kisiasa tarehe saba wiki ijayo.