Kambi ya Syria : Sikujiunga na IS nilikuwa na miaka 10 tu

  • | BBC Swahili
    245 views
    Kufuatia kushindwa kwa kundi la Islamic State (IS) mwaka wa 2019, makumi ya maelfu ya watu, wakiwemo wanawake na watoto wengi, walizuiliwa wakati eneo linaloshikiliwa na IS nchini Syria lilipochukuliwa tena. Wengi ni raia wa kigeni. Mmoja wao ni "Asim", 19, kutoka Tunisia, ambaye alikuwa na umri wa miaka 10 tu aliposafiri kwenda Syria na kaka yake, ambaye alijiunga na IS. Mwandishi wa BBC Persian Nafiseh Kohnavard alipewa fursa adimu ya kutembelea kambi na vituo vya kizuizini kaskazini mwa Syria. #bbcswahili #syria #vita