Halima Mbwana: “Baada ya ajali ile kutokea muda ule ule nilipoinuka niliona mkono umeshakatika”

  • | BBC Swahili
    640 views
    Halima Mbwana alikuwa mmoja kati ya madereva wachache wa mabasi yanayoenda mikoani lakini ndoto yake ilififia ghafla mara baada ya kupata ajali na kupoteza mkono mmoja. Lakini anasema kutokana na kuipenda sana kazi yake hajakata tamaa bado na anaamini atarudi katika sekta ya usafiri kwa namna yeyote hata kukatisha tiketi au kuendesha malori atakapofanikiwa kupata mkono wa bandia ambao anautarajia ukisimamiwa na Waziri wa Maendeleo ya Jamii, jinsia, wanawake na makundi maalumu@gwajimad Mwandishi wa BBC Veronica Mapunda amezungumza naye na kutuandalia taarifa hii Video: Eagan salla #bbcswahili #wanawake #tanzania