Mshukiwa wa mauaji ya dereva wa magari ya safari rally Asad Khan, Maxine Wahome afikishwa mahakamani

  • | Citizen TV
    2,216 views

    Hatma ya mshukiwa wa mauaji ya dereva wa magari ya safari rally Asad Khan, Maxine Wahome bado haijulikani baada ya mkurugenzi wa mashtaka kukosa kutoa mwelekeo kuhusu kesi. Afisa w aupelelezi ameieleza mahakama kuwauchunguzi kuhusu kesi hiyo umekamilika na faili kuwasilishwa kwa mkurugenzi wa mashtaka kupendekeza makosa. Maxine Wahome whajafunguliwa mashtaka yoyote kufikia sasa, jambo ambalo limepingwa na wakili wa familia ya Assad Khan, Danstan Omari. Haya ni huku mmiliki wa nyumba ambako wawili hao walikuwa wakiishi akiiomba mahakama kuruhusiwa kukodisha nyumba hiyo kwani kufikia sasa anakadiria hasara ya shilingi 269,500. Hata hivyo, afisa w aupelelezi amesema kuwa hayo yatafanyika Wahome atakapofunguliwa mashtaka. Mahakama itatoa aumuzi wake tarehe 15 mwezi ujao.