DP Gachagua asema serikali haiwezi kuongeza mgao wa kaunti

  • | Citizen TV
    1,168 views

    Naibu Rais Rigathi Gachagua ameshikilia kuwa serikali haiwezi kutosheleza matakwa ya Baraza la magavana kuhusu mgao wa fedha kwa serikali za kaunti. Rigathi badala yake amewataka magavana kuridhika na shilingi bilioni 385 zilizoahidiwa na serikali kuu. Akizugumza wakati kufunga kongamano la maseneta huko Mombasa Naibu Rais amedai kuwa hali mbaya ya uchumi imechangia hatua hiyo na kuwa Rais William Ruto anatazamiwa kukutana na Baraza la magavana wiki kesho kutatua mzozo huo