Hazina ya bima ya matibabu nchini kubadilishwa kuwa NSHIF

  • | Citizen TV
    843 views

    Hazina ya bima ya matibabu ya NHIF itabadilishwa na kuwa hazina ya bima ya afya ya kijamii NSHIF- ili kuwafaidi wakenya wa tabaka mbali mbali hasa wasiojiweza. Waziri wa afya Susan Nakhumicha ametangaza kuwa hazina hiyo mpya itakayoanza kutekelezwa Julai mosi mwaka huu itahakikisha kuna fedha zaidikugharamia matibabu ya wagonjwa wa aina yoyote hasa wanaougua saratani. haya ni huku ikiarifiwa kuwa kati ya watu watatu wanaougua saratani, wawili hufariki kwasababu ya kuanza matibabu baada ya ugonjwa kuenea zaidi