Mpaka wa Kenya - Somalia kufunguliwa katika kipindi cha miezi 2

  • | Citizen TV
    2,763 views

    Waziri wa Usalama wa kitaifa Prof. Kithure Kindiki amedokeza kwamba katika kipindi cha miezi miwili ijayo huenda serikali ikafungua mpaka wa Kenya na Somalia eneo la Mandera. Mpaka huo umesalia kufungwa kwa zaidi ya miaka kumi kutokana na tishio la usalama. Katika ziara yake ya siku mbili kaskazini mashariki mwa Kenya, Kindiki pia amewaelekeza maafisa wa usalama kuwashirikisha wananchi katika oparesheni za kuwasaka na kuwakabili magaidi wa Al Shabaab.