#WorldCancerDay2023 I Kupuuza kupimwa mapema kwatajwa kama sababu kuu ya ongezeko la vifo

  • | KBC Video
    12 views

    Mapuuza ya watu wengi kwenda kupimwa mapema kwa ugonjwa wa saratani imetajwa kuwa mojawapo ya sababu kubwa ya kuongezeka kwa vifo vinavyotokana na ugonjwa huo hatari. Wakati wa hafla ya ya kuadhimisha siku ya saratani duniani, wataalamu wa maswala ya afya nchini wametoa wito kwa wakenya kujizoesha kujitokeza kupimwa mapema ili kuzuia vifo vinavyosababishwa na ugonjwa wa saratani nchini. Takwimu kutoka taasisi ya kitaifa ya kushughulikia ugonjwa wa saratani nchini zinaonyesha kuwa asilimia sabini ya wagonjwa wa saratani nchini hupoteza maisha huku asilimia thelathini wakinusurika hali ambayo wataalamu wa afya wanasema inapaswa kubatilishwa.

    Connect with KBC Online; Subscribe to our channel: https://t.ly/86BKN Follow us on Twitter: https://twitter.com/KBCChannel1 Find us on Facebook: https://www.facebook.com/kbcchannel1news Check our website: https://www.kbc.co.ke/

    #KBCchannel1 #WorldCancerDay2023 #dirayamagwiji