Katibu mkuu wa ODM aungana na viongozi wengine wa chama kuwashutumu wabunge wa ODM kutoka nyanza

  • | K24 Video
    443 views

    Katibu mkuu wa chama cha ODM Edwin Sifuna ameungana na viongozi wengine wa chama hicho kuwashutumu wabunge wa ODM kutoka nyanza waliozuru ikulu ya Nairobi na kufanya kikao na rais William Ruto hiyo jana. Sifuna anasema sababu wanazotoa ambazo wanadai zilisababisha ziara yao ya ikulu hazina msingi huku akiwataja kama waliokosa uaminifu. Muungano wa Azimio umeandaa kongamano la siku mbili la wabunge wake kuanzia kesho huku ikitarajiwa kuwa suala la utovu wa nidhamu miongoni mwa baadhi ya wabunge litajadiliwa