Waziri Zacharia Njeru azuru kaunti ya Lamu kutathmini changamoto za maswala ya ardhi

  • | Citizen TV
    148 views

    Waziri wa ardhi humu nchini Zacharia Njeru amezuru kaunti ya Lamu kutathmini changamoto za maswala ya ardhi miongoni mwa wakaazi wa Lamu. Ziara yake inajiri siku nne baada ya Raisi William Ruto kuhudhuria Hafla ya maombi eneo la Mpeketoni ambapo baadhi ya viongozi wa Lamu walishinikiza serikali ya kitaifa kuingilia kati na kutatua tatizo sugu la mashamba lamu ili wakaazi wapate hatimiliki.