Mkurugenzi wa zamani wa CID Joseph Kamau apendekeza mafunzo zaidi ya Saikolojia kwa polisi

  • | Citizen TV
    1,208 views

    Aliyekuwa mkurugenzi wa idara ya upelelezi wakati wa utawala wa hayati rais mstaafu Mwai Kibaki, Joseph Kamau ametoa wito kwa idara ya polisi kujumuisha somo la Saikolojia katika mafunzo ya maafisa wanaojiunga na kikosi cha polisi. Hii anasema itasaidia pakubwa kukabili matatizo ya msongo wa mawazo yanayoshuhudiwa miongoni mwa polisi. Kamau amezungumza katika eneo la gatundu alikoenda kuwahamasisha wanafunzi kuhusu utendakazi wa polisi na usalama wao.