Kenya: Raila aongoza maandamano kwa wiki ya pili kulaani kupanda gharama ya maisha

  • | VOA Swahili
    5,430 views
    Kiongozi wa upinzani nchini Kenya Raila Odinga ameongoza maandamano kwa wiki ya pili kupinga kupanda kwa gharama za maisha na kutaka haki katika mfumo wa uchaguzi. Makamu wa Rais wa Marekani Kamala Harris amekutana na Rais wa Ghana wakati taifa hilo linakabiliwa na misukosuko. Matangazo ya Duniani Leo kutoka idhaa ya kiswahili ya Sauti Amerika, Washington, D.C. #habari #VOASwahili Sauti ya Amerika - Idhaa ya Kiswahili inawafikia zaidi ya watu milioni 100 wanaotembelea tovuti, mitandao ya kijamii, radio na televisheni zetu. Tunawasilisha maudhui kuhusu Afrika Mashariki na Kati kwa nchi takriban 11 huko Afrika na wale walioko ughaibuni na kwingineko duniani. Vipindi vyetu vimejikita katika maudhui mbalimbali ikiwemo habari, vijana, wanawake, siasa, sayansi, teknolojia, afya, biashara, michezo, muziki na burudani na pia tunawashirikisha wasikilizaji wetu.