EACC inatilia shaka uadilifu wa IEBC

  • | K24 Video
    99 views

    Tume ya uchaguzi na mipaka nchini IEBC inaliomba jopo la majaji watatu walioteuliwa na jaji mkuu Martha Koome kufanya uamuzi mapema kuhusu hatma ya wawaniaji waliotajwa katika kesi za ufisadi kabla ya muda wa kuchapishwa kwa karatasi za kura. Kulingana na mwenyekiti wa IEBC wafula Chebukati, tume hiyo haina uwezo wa kuwazuia wagombea hao kushiriki uchaguzi iwapo wamekata rufaa ya kesi zao. Vilevile Chebukati amepokea ripoti iliyochapishwa na tume ya kukabiliana na ufisadi nchini EACC, ambayo anasema itaisaidia tume hiyo kufanya maamuzi ya kuwapa wawaniaji tiketi za kuwa debeni.