Raila awalaumu Rais Ruto na naibu wake kwa vurugu

  • | Citizen TV
    5,469 views

    Viongozi wa muungano wa azimio sasa wanamtaka Rais William Ruto kuwajibikia matukio yaliyoshuhudiwa wakati wa maandamano ya siku ya Jumatatu. Viongozi hao wakiongozwa na raila odinga wamesuta serikali kwa kile walichodai ni kufadhili vurugu vilivyoshuhudiwa dhidi yao, wafuasi wao pamoja na uvamizi na uharibifu wa mali ya familia ya rais mstaafu Uhuru Kenyatta.