Naibu rais Gachagua ataka biashara zifunguliwe kesho kama kawaida

  • | K24 Video
    240 views

    Naibu rais Rigathi Gachagua amesisitiza kuwa serikali italinda mali ya wakenya wakati wa maandamano, iwe ni ya mabwanyenye au walalahoi.hakikisho hilo limejiri siku mbili baada ya uvamizi katika shamba la Northlands linalomilikiwa na familia ya Kenyatta, pamoja na kampuni ya Spectre inayomilikiwa na kinara wa Azimio Raila Odinga wakati wa maandamano ya jumatatu. Gachagua ametoa hakikisho hilo akiwa Nyeri.