Vijana waraiwa kukumbatia kilimo kaunti ya Kilifi

  • | Citizen TV
    216 views

    Licha ya idadi ya vijana wanaojihusisha na kilimo biashara kuongezeka, serikali ya kaunti ya kilifi kupitia idara ya kilimo sasa imeanza hamasa ya kuwahusisha vijana katika kilimo biashara ili kujikimu kibiashara na kuongeza uzalishaji chakula kaunti hiyo. Afisa mkuu idara ya kilimo kaunti hiyo sasa amewarai vijana kuasi dhana ya kuwa kilimo ni shuhuli ya wazee. serikali imeanza kuwapa pembejeo na fedha za kuwasaidia kuendeleza kilimo. Hata hivo vijana ambao tayari wamekua wakijishuhulisha na kilimo wameelezea jinsi maisha yao yameimarika kutokana na kilimo biashara.