Rais Ruto asisitiza kuwa hakutakuwa na handisheki

  • | K24 Video
    178 views

    Rais William Ruto ameweka wazi kuwa hakutakuwa na handisheki baina yake na kinara wa Azimio la Umoja Raila Odinga. Rais amesema hayo nchini Rwanda akijibu maswala ya wanahabari pamoja na mwenyeji wake rais paul kagame wa Rwanda. Ruto ameeleza kuwa handisheki ya 2018 haikuwa na matokeo mazuri kwani hakuna aliyekosoa serikali na kuitaka kuwajibika. Hata hivyo ameeleza kutakuwa na mazungumzo ya uzalendo kati ya pande zote mbili kuangazia maswala yaliyowasilishwa na upinzani. rais yuko rwanda kwa ziara ya siku mbili.