Naibu Rais Rigathi Gachagua aongoza kikao cha wadau wa kahawa katika kaunti ya Meru

  • | Citizen TV
    263 views

    Naibu Rais Rigathi Gachagua anaongoza kikao cha wadau katika sekta ya kahawa, kuzungumzia kilimo cha zao hilo ambalo limekabiliwa na changamoto nyingi siku za hivi karibuni. Katika mkutano huu uliowajumuisha mawaziri watatu ikiwemo waziri wa kilimo, waziri wa biashara na waziri wa vyama vya ushikika, wataalamu wa ukulima wa kahawa, viongozi wa kisiasa na wakulima, Gachagua amesema kuwa liwe liwalo, lazima serikali italeta mabadiliko katika sekta ya kahawa. Kadhalika, imebainika kuwa kilimo hicho kimepungua ikilinganishwa na miaka ya hapo awali huku malipo duni yakitajwa kama sababu kuu ya upungufu huu.