Joe Githahi na mpenziwe Kate Ngaine watarajiwa kufunga pingu za maisha mwezi ujao

  • | Citizen TV
    1,005 views

    Familia na marafiki wa seneta wa kuteuliwa Betty Montet walijumuika katika sherehe ya kukaribisha mchumba wa mwanawe ijulikanayo kama itara, nyumbani kwao Maanzoni kaunti ya Machakos. Mwenyekiti wa Royal Media Services daktari S.K. Macharia, naibu mwenyekiti Gathoni Macharia, walijumuika na familia hiyo kushuhudia hafla hiyo kumpa baraka bwana harusi Joe Githahi na mpenziwe Kate Ngaine wanaotarajiwa kufunga pingu za maisha mwezi ujao.