Mashambulizi ya kigaidi Lamu

  • | Citizen TV
    1,153 views

    Shambulizi la Jumamosi usiku katika vijiji viwili kaunti ya Lamu iliyosababisha kuuawa kwa watu watano limezua masuali mengi kuhusu hali ya usalama nchini. Kisa hicho kikiashiria kuongezeka kwa visa vya mashambulizi ya ugaidi ambavyo vimeshuhudiwa katika kaunti za Lamu, Mandera, Garissa na Wajir na ambavyo vimesababisha kuuawa kwa zaidi ya watu 29 mwaka huu, wengi wao wakiwa maafisa wa usalama.