Hospitali ya Nairobi Women's yajitetea na madai yaliyotolewa na shirika la Oxfam

  • | Citizen TV
    503 views

    Hospitali ya Nairobi Womens imekana ripoti iliyotolewa na shirika la Oxfam International kuhusu shughuli zake. Kupitia kwenye taarifa kwa vyombo vya habari Afisa Mkuu Daktari Sam Thenya amesema hospitali hiyo haijawazuia wagonjwa kwa misingi yoyote na kwamba inafuata uamuzi wa mahakama mwaka 2018 kuhusu swala hilo. Aidha amesisiitiza kuwa hospitali hiyo haijapokea fedha zozote kutoka kwa mashirika ya uwekezaji mbali na hayo hakuna fedha zilizotolewa na mashirika hayo kwa hospitali hiyo ili kupunguza gharama ya matibabu. Na kuhusu umiliki wa hospitali hiyo Daktari Thenya amesisitiza kuwa tangu mwaka 2006 hazina ya Afrika Health ilipowekeza katika hospitali hiyo kwa mara ya kwanza kumekuwa na wawekezaji wengine waliojihusisha na shughuli zake. na kwamba makubaliano hayo ni ya kibiashara na kumekuwa na makubaliano ya kuwepo kwa wenye hisa na yalifuata taratibu zilizoko za kisheria za humu nchini za kimataifa.