Mhisani katika kaunti ya Busia ajitolea kuwajengea wajane makazi bora

  • | Citizen TV
    581 views

    Wajane na katika eneo bunge la Matayos kaunti ya Busia wana kila sababu ya kutabasamu baada ya kuanzishwa kwa mradi wa kuwajengea nyumba al maarufu Houses of Hope. Kukithiri kwa umasikini miongoni mwa wajane katika eneo hilo la Matayos kumesababisha mhisani mmoja mkazi wa Busia kwa ushirikiano na jamii kuwajengea wajane nyumba za udongo kama njia ya kuwastiri katika mazingira salama baada ya kufiwa na waume zao.