Utumizi wa mihadarati wasalia kuwa changamoto kubwa katika eneo la Pwani

  • | Citizen TV
    280 views

    Utumizi wa mihadarati umesalia changamoto kubwa si tu kwa serikali bali kwa familia nyingi za waraibu hawa. Tatizo la utumizi wa mihadarati mara nyingi huathiri watumizi na hata familia za wanaotumia dawa hizi kukidhi uchu wao na mara nyingi hata kusababishia familia nyingi umaskini. Lakini hata katika lindi hili la mihadarati, kuna wale ambao wamemudu kujinasua kutoka kwenye minyororo hii.