Mrengo wa Upinzani watumia sabasaba kushinikiza mabadiliko katika mswada wa Fedha 2023/2024

  • | Citizen TV
    616 views

    Mrengo wa upinzani nchini umetoa tahadhari kuhusu uasi mkubwa wa umma unaolenga serikali kuhusiana na kutia saini kuwa sheria mswada wa Fedha wenye utata wa 2023/2024.Gavana wa Siaya James Orengo na Mbunge wa Rarieda Otiende Amollo, wameeleza kuwa kuna miadi na serikali siku ya Ijumaa, maadhimisho ya siku ya Saba Saba watakapozindua mikakati inayolenga kuwajibisha serekali ya Kenya Kwanza kuhusu mahitaji ya msingi ya wakenya.Wakizungumza katika Kanisa la St Paul’s ACK Lihanda katika eneo bunge la Gem, wanaeleza kuwa inasikitisha sana kwamba mishahara ya Wakenya itapunguzwa kwa asilimia 1.5 kutekeleza miradi ya ujenzi wa nyumba na wawekezaji pia hawatasazwa, kwani watatozwa ushuru kwa kila uwekezaji wanaoweka nchini.