Mawakili waandamana Kisii kulalamikia huduma zisizoridhisha katika ofisi ya msajili wa mashamba

  • | Citizen TV
    772 views

    Wanachama wa muungano wa mawakili tawi la Magharibi mwa Kenya wanaandamana mjini Kisii kulalamikia huduma zisizoridhisha katika ofisi ya msajili wa mashamba kaunti ya Kisii. Mawakili hao wanasema imekuwa vigumu kupata huduma kwao na hata kwa wananchi baada ya afisa mgeni katika ofisi ya msajili wa mashamba kuchukua hatamu ya uongozi kando na kusitisha huduma za mitandao. Hata hivyo afisa huyo kwa jina Charles Ayienda ameshikilia kwamba nia yake ni kuziba mianya ya ufisadi.