Rais Ruto asema Kenya imeondoa viza za usafiri kati ya Kenya na Comoro

  • | Citizen TV
    789 views

    Rais William Ruto ametangaza kuwa kenya itaondolea mbali mahitaji yoyote ya viza kwa raia wa visiwa vya Comoro wanaozuru humu nchini. Ruto ameyasema hayo alipohudhuria maadhimisho ya 48 ya uhuru wa taifa hilo. Kwenye hotuba yake wakati wa maadhimisho hayo, Rais Ruto pia aliahidi ushirikiano wa kiuchumi na kidiplomasia kati ya Kenya na Comoro. Alipongeza uongozi wa Rais Azali Assoumani wa Comoro huku akitoa mwaliko kwa nchi hii kujiunga na Jumuiya ya Afrika Mashariki.