Katibu wa Kawi Alex Wachira atetea kupanda kwa gharama ya umeme nchini

  • | Citizen TV
    115 views

    Huku wakenya wakiendelea kulalamikia kupanda kwa gharama ya bei ya umeme, serikali inashikilia kuwa nyongeza hii imechangiwa pakubwa na kupanda kwa dola na hata wizi wa umeme unaoendelezwa nchini. Katibu katika Wizara ya Kawi Alex Wachira akisema kuwa, wanaendelea kuweka mikakati kupunguza wizi wa umeme ili kusaidia kuimarisha bei yake. Alikuwa akizungumza wakati wa kipindi cha sema na citizen hii leo.