Mameneja watatu wa kampuni ya Jibini ya Browns wakamatwa

  • | Citizen TV
    846 views

    Wasimamizi watatu wakuu wa kampuni ya kutengeza jibini ya Brown's iliyo Tigoni, kaunti ya Kiambu wanatarajiwa kufikishwa mahakamani hapo kesho kufuatia madai ya kuwadhalilisha wafanyakazi wa kike katika kampuni hiyo. Watatu hao wanaidawa kuwalazimisha wanawake hao kuvua nguo wakitaka kujua ni nani kati yao alikuwa kwenye hedhi, baada ya sodo iliyotumika kupatikana kwenye mazingiya yake.