Watu 5 wafariki kufuatia ajali mbili tofauti barabarani

  • | Citizen TV
    1,399 views

    Watu watano wamefariki katika ajali mbili tofauti za barabarani katika kaunti za Marsabit na Bomet. Kwenye ajali ya kwanza ambulensi iliyokuwa inatoka marsabit kuelekea sololo ilipoteza mwelekeo na kubingiria mara kadhaa eneo la Bubissa kwenye barabara kuu ya Marsabit - moyale na kumgonga mhudumu wa bodaboda aliyekuwa amebeba abiria na kufariki papo hapo. Wawili hao walifariki pamoja na mhudumu wa afya aliyekuwa katika ambulensi. Kisa hiki kimethibitishwa na kamanda wa polisi kaunti ndogo ya Turbi Isaac Ahmed. Kwingineko katika kaunti ya Bomet, watu wawili wamefariki na watatu kujeruhiwa kufuatia ajali iliyotokea eneo la mulot kwenye barabara ya Bomet kuelekea Narok.