Idara ya Afya yatengewa Shilingi Bilioni 2.9 kwenye bajeti ya kaunti ya Kwale

  • | Citizen TV
    81 views

    Idara ya afya kaunti ya Kwale imetengewa mgao mkubwa wa bajeti ya kaunti hiyo kwenye mwaka wa kifedha wa 2023/2024. Idara hiyo ikipokea shilingi bilioni 2.9. huku Idara za elimu na maji zikipokea bilioni 1.5 na bilioni 1.3 mtawalia. Gavana Fatuma Achani akiahidi kuimarisha huduma za afya kaunti hiyo ili kuhakikisha wakaazi hawahangaikii matibabu. Aidha, Gavana Achani amesema miradi ya maendeleo ya kaunti itachukua asilimia 40 ya bajeti hiyo huku asilimia 59 ikiendea matumizi ya serikali, mishahara na basari.