Kamati inayochunguza mauaji ya Shakahola yamhoji Waziri wa Usalama Kithure Kindiki

  • | Citizen TV
    103 views

    Waziri wa Usalama Profesa Kithure Kindiki leo anafika mbele ya kamati maalum ya Bunge la Seneti inayochunguza matukio ya Shakahola. Waziri Kindiki anafika mbele ya kamati hiyo kuhusiana na kuhamishwa kwa maafisa wa Usalama wakati matukio ya Shakahola yalipojitokeza. Haya yakijiri siku moja baada ya awamu ya nne ya ufukuaji wa maiti kuendelea shakahola, ambapo miili 12 ilifukuliwa, huku ikiaminika kuwa watu zaidi walizikwa kwenye makaburi 40 zaidi yanayolengwa.