Asilimia 90 ya hoteli eneo la Diani katika kaunti ya Mombasa yaendelea kupokea wageni

  • | Citizen TV
    102 views

    Kwa kawaida kipindi cha Aprili baada ya sherehe za Pasaka hadi mwezi Julai, sekta ya utalii hushuhudia shughuli chache na kusababisha hoteli nyingi eneo la Pwani kufungwa. Lakini hali hii imeanza kubadilika kwani zaidi asilimia 90% ya hoteli eneo la Diani kaunti ya Kwale zilisalia wazi kwa wageni na kuonyesha ukakamavu katika kipindi hiki.