Raila Odinga awalaumu polisi kwa vifo na uharibifu wa mali

  • | Citizen TV
    5,143 views

    Kinara wa Azimio la Umoja Raila Odinga amewalaumu maafisa wa polisi kwa fujo, uharibifu wa mali, na vifo vilivyoshuhudiwa kwenye maandamano ya leo kote nchini. Raila amesisitiza kuwa hatalegeza kamba kwenye shinikizo zake za kuitaka serikali ya rais william ruto kukomesha unyanyasaji wa raia na ukandamizaji wa kiuchumi unaopaniwa kutekelezwa kupitia ushuru maradufu ambao utaongeza maradufu bei ya bidhaa muhimu.