Jamii ya Kisii bado inaendelea na ukeketaji wa wasichana

  • | Citizen TV
    234 views

    Hofu inazidi kughubika wadau mbalimbali kaunti ya Kisii kutokana na ukeketaji wa watoto wasichana walio na umri wa kati ya miezi miwili na miaka mitano. Hali hii ikisababisha mkutano wa dharura wa waakilishi wa mashirika ya kijamii, maafisa wa serikali na wale kutoka wizara ya afya. Kama anavyotuarifu Chrispine Otieno hadi sasa eneo la Gusii lingali na asilimia 84 ya ukeketaji wa watoto.