- 238 viewsDuration: 1:38Sekta ya kilimo inajiandaa kwa mageuzi makubwa baada ya wadau wa viwanda kuafikiana kushirikiana na vyuo vya ufundi na mafunzo ya kiufundi, TVET. Katika kikao cha juu kilichofanyika Meru, wadau walikubaliana kutumia mfumo wa Dual TVET ili kuwapa vijana ujuzi wa vitendo na kuondoa pengo la ajira kwenye sekta hii muhimu kwa uchumi.