Uvamizi wa ndovu unawapa tumbo joto wakaazi wa Mwangea kwa Dadu kaunti ya Kilifi

  • | Citizen TV
    111 views

    Uvamizi wa ndovu kwenye mashamba na makaazi ya wanakijiji eneo la Mwangea kwa Dadu kaunti ya Kilifi unawapa tumbo joto wakaazi eneo hilo baada ya uvamizi wa hivi punde kuwaacha na hasara kubwa huku mtu mmoja akiripotiwa kufariki na mashamba yao kuharibiwa. Wakaazi hao wanatishia kuandamana iwapo hatua za dharura hazitachukuliwa na idara ya huduma kwa wanyamapori -KWS.