Wakulima kutoka kaunti ya Trans Nzoia wataka mahindi yanunuliwa shilingi 6,000

  • | Citizen TV
    986 views

    Wakulima katika kaunti ya Trans Nzoia wanaitaka halmashauri ya nafaka na mazao kununua mahindi wanayovuna kwa shilingi elfu sita na zaidi kwa kila gunia la kilo tisini. Wakulima wanasema kuwa japo mbolea ya bei nafuu inayotolewa na serikali imesaidia kupunguza gharama ya uzalishaji mahindi kwa shilingi elfu kumi kwa kila ekari moja, gharama ya mafuta na gharama zinginezo bado zimeendelea kuwa juu. Haya yanajiri wakati ambapo serikali inasema bei ya unga itarudi chini karibuni.

    gun