Jopo la majaji watatu wa Mahakama Kuu laskiza kesi kuhusu sheria ya fedha ya mwaka 2023/24 [Part 1]

  • | Citizen TV
    4,173 views

    Jopo la majaji watatu limeanza kusikiza kesi kuhusu sheria ya fedha ya mwaka 2023/24. Makundi mbalimbali ya wanaharakati na seneta wa Busia Okiya Omtatah waliwasilisha kesi kupinga utekelezaji wa sheria hiyo. Jaji Mugure Thande aliagiza sheria hiyo isitekelezwe, lakini jopo la majaji watatu wa mahakama ya rufaa wakabatilisha uamuzi huo baada ya serikali kudai kuwa inashindwa kutekeleza majukumu yake kutokana na ukosefu wa fedha. Jaji David Majanja, Christine Meoli na Lawrence Mugambi wanasikiza kesi ya leo.