Wanawake wafunzwa umuhimu wa kunyonyesha katika kaunti ya Baringo

  • | Citizen TV
    102 views

    Mashirika mbalimbali yanayoshughulikia urutubisho wa lishe bora yalikongamana katika eneo la Tangablui Mashariki yakilenga kuwapatia kina mama msaada wa chakula ili kudhibiti utapiamlo, jambo walilosema litasaidia wanawake kupata nishati ya kunyonyesha. Aidha walitaka wanawake kunyonyesha hadi miezi sita huku wakikemea mila potovu inayochangia kutonyonyesha baina ya wanawake.