Watu watatu wafariki kufuatia ajali ya barabarani eneo la Ngata bridge kaunti ya Nakuru

  • | Citizen TV
    101 views

    Watu watatu wamefariki kufuatia ajali ya barabarani iliyotokea mapema leo katika eneo la Ngata bridge kaunti ya Nakuru. Ajali hii ilitokea wakati matatu iliyokuwa imebeba abiria kutoka mjini Eldoret kuelekea Nairobi kugongana na lori. Abiria watatu waliokuwa kwenye matatu hiyo waliaga, miongoni mwao akiwa mtoto mdogo. Watu wengine 11 walijeruhiwa na wameendelea kutibiwa katika hospitali ya Nakuru.