Viongozi wa kidini wapongeza serikali na upinzani kwa kuongea

  • | Citizen TV
    890 views

    Viongozi wa kidini wamepongeza mazungumzo kati ya serikali na upinzani wakiutaja kama hatua kubwa ya kurejesha hali ya utulivu nchini. Wakiongozwa na Askofu Martin Kivuva wa kanisa Katoliki Dayosisi ya Mombasa, viongozi hao wametaka mazungumzo hayo kujumuisha maswala muhimu kama vile amani, kupambana na kero ya umaskini,ukosefu wa jaira na ufisadi.