Familia yadai haki baada ya mwana wao kujeruhiwa ziarani

  • | Citizen TV
    1,881 views

    Familia moja katika eneo la Githurai 44 hapa jijini Nairobi inatafuta haki ya mwana wao ambaye anauguza majeraha mabaya katika hospitali ya rufaa na mafunzo ya chuo kikuu cha Kenyatta. Mtoto huyo wa gredi ya kwanza katika Shule ya Green Angels alihusika katika ajali wakati alipokuwa amezuru eneo moja la burudani na wanafunzi wenzake siku ya jumanne wiki hii.