Wadau katika kaunti ya Migori waanda kongamano maalum kutafuta mbinu za kumaliza ukeketaji

  • | Citizen TV
    174 views

    Baadhi ya wanaharakati wa kupinga ukeketaji katika Kaunti ya Migori wameanza kampeni mpya dhidi ya tamaduni hiyo katika eneo la Kuria. Wanaharakati hao wakiongozwa na mke wa gavana wa kaunti ya Migori Agness Ochilo wameandaa kongamano la siku nne ambalo limewaleta pamoja wasichana zaidi ya 200, wazee na maafisa wa usalama miongoni mwa wadau wengine.