Aliyekuwa rais wa Marekani Trump atuhumiwa kwa kujaribu kuvuruga matokeo ya uchaguzi

  • | Citizen TV
    762 views

    Aliyekuwa rais wa Marekani Donald Trump na washirika wake 18, wamepatikana na mashtaka ya kujibu katika jaribio lao la kutaka kubatilisha matokeo ya uchaguzi mkuu mwaka 2020, katika jimbo la Georgia. Trump na washirika wake wanashutumiwa kwa kujaribu kuvuruga matokeo ya uchaguzi katika jimbo la Georgia ambalo alishindwa na rais Joe Biden. Trump anadaiwa kumshurutisha msimamizi wa uchaguzi katika jimbo hilo, kutafuta kura za kutosha kumpa ushindi ili aendelee kusalia madarakani.