Naibu rais Rigathi Gachagua atarajiwa kufunga kongamano la ugatuzi linaloendelea mjini Eldoret

  • | Citizen TV
    172 views

    Naibu wa rais Rigathi Gachagua anatarajiwa kufunga rasmi kongamano la ugatuzi linaloendelea mjini Eldoret kaunti ya uasin Gishu. Kongamano hilo la siku tatu linalokamilika leo limeangazia masuala mbalimbali ya ugatuzi huku njia mwafaka za kuboresha serikali za kaunti zikijadiliwa. Brenda Wanga amekuwa akihudhuria kongamano hilo tangu siku ya Jumatano na sasa tunaungana naye mubashara kutoka mjini Eldoret kwa mengi zaidi.