Tume ya madili nchini, EACC yataka mamlaka ya kuwakamata na kuwashtaki wafisadi

  • | Citizen TV
    187 views

    Tume ya maadili na kupambana na ufisadi nchini EACC, ina mpago wa kuwasilisha hoja bungeni ili kubadilisha sheria na kuipa mamlaka ya kuwakamata na kuongoza mashtaka ya washukiwa wa ufisadi. Akizungumza jijini Mombasa kwenye kongamano la makarani, mwenyekiti wa EACC Askofu David Oginde pia ameeleza wanahabari kuwa tume hiyo inawalenga hata wanaohusishwa na ufisadi wa kiwango kidogo.