EACC yapendekeza magavana wawili watiwe mbaroni

  • | Citizen TV
    2,153 views

    Wakati serikali za kaunti zikiadhimisha miaka kumi ya ugatuzi katika kongamano mjini Eldoret, tume ya kupambana na ufisadi EACC imetoa ripoti ya ufisadi katika baadhi ya magatuzi. katika ripoti yake, EACC imechapisha majina ya magavana ambao wana kesi za ufisadi kortini baadhi yao wakiwa ofisini kwa sasa na wengine ambao wamestaafu au kushindwa katika uchaguzi.